Katika makala yangu ya leo nimekuwekea mambo muhimu ya kufuata ili uweze kufanikiwa
Kila binadamu anatamani kupata mafanikio katika mambo anayofanya, kutokana na utafiti nilioufanya haya ndo mambo kuu ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia kufikia malengo au mafanikio yako
- Tafuta utajiri
Tunaposema utajiri, hatuongele pesa wala heshima.
Utajiri ni kuweza kuwa na vyanzo mbalimbali vinavyoweza kukuingizia kipato bila ya wewe kuwepo.
Pesa ni matokeo ya muda na utajiri, vilevile heshima ni nafasi yako katika jamii.
Kwahiyo ni vyema kuwekeza katika vitu ambavyo vitakutengenezea pesa wakati wewe umelala.
Mfano: Kununua hisa katika kampuni, kutengeneza blog, kutengeneza video za YOUTUBE, Kujenge fremu za kupangisha, NK.....
2. Achana na watu/marafiki na kelele za mitandaoni
Marafiki wengi ndio wanaongoza kwa kukatishana tamaa na kurudisha maendeleo nyuma.
watakukatisha tamaa kuwa jambo flani haliwezekani au usifanye hivi ama vile.
Simamia katika kitu unachokiamini, achana na kelele za mitandaoni wekeza muda wako katika maisha yako, hii itakusaidia kufika mbali.
3. Huwezi kuwa tajiri kwa kuazima/kuuza muda wako
Ni lazima umiliki/ufanye biashara, lazima uwekeze katika vyanzo vingine vya mapato ili uweze kupata uhuru wa kifedha
3. Utajiri upo katika jamii inayokuzunguka
Utapata utajiri kwa kutoa huduma au kwa kutatua matatizo yaliyopo katika jamii inayokuzunguka na kuipatia jamii inachokitaka na sio unachokitaka wewe.
(Tafuta kitabu kinaitwa mgodi by Amosi Nyanda)
4. Chagua niche/ujuzi uijue kwa undani sana
Chagua ujuzi au taaluma ukomae nayo mwanzo mwisho uweze kuielewa vizuri. Hiyo taaluma itakusaidia kufika mbali.
Mfano: kama ni biashara hakikisha umeielewa na kuifanyai tafiti vizuri
Interned ndio sehemu ambayo unaweza kujifunza mambo yote na kufanyia majaribio mitandaoni.
5. Penda kitu unachokifanya
Wengi hupenda kusema wanafanya kazi wanayoipenda lakini ukweli ni kwamba unatakiwa upende kazi unayoifanya. Hii itakusaidia kuweza kujifunza zaidi na kujiongeza katika hicho unachokifanya na kuongeza umakini zaidi.
6. Chagua washirika wenye kiu ya mafanikio
Hii ni hatua muhimu sana, Usikubali kufanya kazi na watu wavivu wenye kukatisha tamaa. Shirikiana na watu wenye nguvu na kiu ya mafanikio katika kila wanayoyafanya.
Vilevile kuwa karibu sana na watu waliofanikiwa, hii itakusaidia kuelewa zaidi njia walizopitia na utajifunza mengi kutoka kwao.
7. Jifunze kuuza/Kujenga
Hata kama hauuzi bidhaa au hufanyi biashara jifunze kuuzaa na kuandika nakara, Hii itakusaidia baadae katika mafanikio yako.
Hapa nakushauri ujifunze copywriting skills
8. Kuwa na ujuzi wa kujilinda
Ujuzi pekee ni ule ambao haujafundishwa darasani, unajifunza mtaani.
Mfano: kuna kozi mbalimbali za kusoma mitandaoni. Ni muhimu kuwa na ujuzi ambao utakusaidia kuingiza kipato.
9. Fanya biashara yako mwenyewe
Fanya biashara mabilimbali, hakikisha una uwezo wa kuzisimamia ili uwezo kujifunza changamoto zake na kuzielewa.
Watu matajiri wote walianza na biashara ndogo sana lakini kutokana na imani yao wameweza kuzikuza mpaka kuwa bishara kubwa sana duniani.
10. Usitamani sana kuajiriwa
Ajira itawafurahisha tu wazazi wako lakini haitakufikisha popote. Jitahidi sana kupata elimu, pata ujuzi na huo ujuzi utumie kuingiza kipato.
Kuna aina mbalimbali za ujuzi ambazo hauhitaji kuwa na pesa.
11. Anza chini na ulichonacho
Kama una smartphone anza na hiyo, simu ya mkononi inatosha kukuingizia laki tano mpaka milioni kwa mwezi, ukiwa na computer ni bora zaidi maana kuna namna nyingi za kuingiza pesa mitandaoni bila kutumia pesa nyingi.
Hakuna ujuzi unaoitwa Biashara, kwahiyo jitahidi sana uepuke na semina za biashara.
Fanya maamuzi sasa tuwasiliane whatsapp (+255757915043)
Comments
Post a Comment