UTANGULIZI
Kuna maandiko mengi
mitandaoni juu ya ufugaji kuku wa kienyeji. Kutokana na hayo maandishi
kutojitosheleza, Nimeandaa mbinu ambazo kwa mikono yangu mwenyewe na kwa msaada
wa vitabu mbalimbali nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji.
Nimeandika hiki kitabu
kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda ya kisasa,
mashine za kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) na
gharama nyinginezo.
Naomba mzijue mbinu hizi,
huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu (wajasiliamali) wale ambao
mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabu
nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni ya kitanzania. Mbinu
zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi na katika maandiko (blogs) za
watu mbalimbali nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa sana, mbinu zingine
nilizigundua mwenyewe katika ubunifu wangu nikafanikiwa sana.
Hizi mbinu hazijafanyiwa
utafiti rasmi wa kisayansi lakini nimeweza kufanikiwa na watu mbalimbali
waliozitumia wameweza kuwa na kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana
kupitia ubunifu huu wa kiasili.
Ewe mjasiliamali nakualika usome makala hii mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kuelewa simulizi zangu zote uweze kuongeza uzoefu katika utunzaji wa kuku.
Katika makala hii nimegusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine, Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Huu ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu vijana wa kitazania ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasiliamali.

![](https://i.ytimg.com/vi/jSwjpFDyz_A/hqdefault.jpg)
https://www.google.com/search?q=kuku+wa+kienyeji&source=lnms&tbm=isch&sa=X&ved=0ahUKEwi_u9fznorNAhWBFxQKHUXSAcMQ_AUICCgC&biw=1366&bih=652
Hiyo makala naipata wapi ndugu?
ReplyDelete