Wanaume wengi wanapopoteza nguvu za kiume hudhani ni tatizo dogo la kawaida au la kiumri, lakini ukweli ni kwamba mara nyingi lina uhusiano wa moja kwa moja na magonjwa ya moyo . Zaidi ya viungo hamsini vya mwili vinashirikiana ili kuhakikisha uume unasimama vizuri, hivyo ikitokea kiungo kimoja hakifanyi kazi yake ipasavyo, mfumo mzima wa usimamishaji wa uume huathirika. Uhusiano kati ya Moyo na Nguvu za Kiume Kwa mwanaume, kupungua kwa nguvu za kiume ni moja ya dalili muhimu za ugonjwa wa moyo . Utafiti unaonesha kuwa wanaume wenye matatizo ya moyo hukumbwa na changamoto kubwa ya kufanya vizuri tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu kusimama kwa uume kunahitaji msukumo wa damu wa kutosha kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mishipa ya uume . Iwapo mishipa ya damu imeziba au moyo umeshindwa kusukuma damu ipasavyo, basi damu haitafika kwa kiwango cha kutosha kwenye uume, na matokeo yake ni kushindwa kusimama vizuri au kupoteza nguvu kabisa. Hii ikimaanisha kwamba, matatizo yoyote ya mo...