Wanaume wengi hupoteza nguvu za kiume si kwa sababu ya uzee pekee, bali kwa sababu ya magonjwa ya mwili. Ukweli ni kwamba, zaidi ya viungo 50 vya mwili vinashirikiana ili kuhakikisha uume unasimama vizuri. Hivyo, ikitokea kiungo kimoja kimeharibika, mfumo mzima wa usimamishaji wa uume huathirika. Kisukari na Nguvu za Kiume Ugonjwa wa kisukari ndio sababu kubwa ya kupungua au kupotea kabisa kwa nguvu za kiume. Tafiti zinaonesha kuwa kati ya asilimia 35–75 ya wagonjwa wa kisukari, hupitia changamoto hii. Wanaume wenye kisukari huanza kupata tatizo hili miaka 10–15 mapema zaidi ikilinganishwa na wasio na kisukari. Umri wa miaka 50–70: Asilimia 50 ya wanaume wenye kisukari hupata upungufu wa nguvu za kiume. Zaidi ya miaka 70: Takribani 95% hupatwa na tatizo hili. Kisukari huathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu, huzuia utengenezaji wa kemikali zinazohitajika kwa kusimama kwa uume, na hivyo husababisha kupun...